Mwimbaji staa anayetamba na wimbo wa ‘Ukivaaje unapendeza?’ Dogo Janja amefunguka akisema sasa ana mpango wa kufanya biashara akitumia Brand yake ya Dogo Janja akidai ataingiza sokoni bidhaa tofauti na nguo.Akizungumza kwenye 255 ya XXL ya Clouds FM Dogo Janja amesema ataingiza sokoni bidhaa zinazowahusu watoto zaidi akidai kuwa na mpango wa kuleta vifaa vya michezo kwa watoto kama game ya Dogo Janja.>>“Brand ya Dogo Janja itakuja lakini mimi sitakuja na Brand ya nguo ila nitakuja na vifaa vya watoto vya michezo vya Dogo Janja. Mimi nitakuwa na-deal na madogo janja zaidi. Hii ipo kama mwezi wa Sita nadhani Mungu akijaalia nitasafiri kwenda kufanya mitikasi. Kwa hiyo, nikirudi narudi na bidhaa.” – Dogo Janja
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment