Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefunguka na kusema Watanzania tumerogwa kwani tuna kila kitu ambacho kinaweza kutufanya kuwa mbele kimaendeleo lakini siku zote tumekuwa nyuma. Mchungaji Gwajima amesema hayo leo wakati akitoa mahubiri yake kwenye kanisa lake na kusema Watanzania wamerogwa kwani wanapenda sana maandamano na vitu visivyo na msingi kuliko kufanya kazi, anasema Tanzania ina vitu na mali nyingi "Ukitaka kuingoza Tanzania lazima uwe na moyo wa mwendawazimu maana watu wake wamerogwa mpaka wamerogeka, ni nchi ya waliorogeka tu unaweza kwenda kusaini mikataba ya madini, nenda kasaini mkataba wa madini Japan au Kenya uone, sisi Tanzania Watanzania tunauza ubuyu na karanga mzungu anabeba kila kitu, sisi tumerogwa. Tanzania ina mito mingi yenye maji lakini maji yanakwenda tu, watu hawalimi" alisema Gwajima Mbali na hilo Gwajima amempa tano Rais Magufuli kwa kitendo chake cha kuzuia makontena ya madini na kusema ni hatua nzuri na Rais ashikirie hapo hapo "Hata kama tulisaini mikataba ya kufa mtu sawa tu Rais ashikirie hapo hapo hakuna kuruhusu makontena mpaka wazungu macho yao yawe mekundu, kama hatujawa tayari kuchimba madini tuyaache kwanza, wapo wanaosema sijui tutashitakiwa, sijui mikataba itatubana ondoka na makaratasi yako hapa yale madini ni ya kwetu, mwanasiasa unayetaka kulia ulie tu na ufe madini hakuna kwenda" alisema Gwajima
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment