1.0 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kuuarifu umma kuwa, mwezi Septemba na Oktoba mwaka 2016 ilifanya uhakiki wa vyuo vyote vya elimu ya juu nchini ili kuhakiki ubora wa elimu inayotolewa vyuoni. Ripoti ya uhakiki ilionesha mapungufu kadhaa katika baadhi vyuo. Kwa sababu hiyo, Tume imesitisha udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18 kwa vyuo vifuatavyo:
- Eckenforde Tanga University
- Jomo Kenyatta University, Arusha
- Kenyatta University, Arusha
- United African University of Tanzania
- International Medical and Technological University (IMTU)
- University of Bagamoyo
- Francis University College of Health and Allied Sciences
- Archibishop James University College
- Archibishop Mihayo University College
- Cardinal Rugambwa Memorial University College
- Kampala International University Dsm College
- Marian University College
- Johns University of Tanzania Msalato Centre
- Johns University of Tanzania, Marks Centre
- Joseph University College of Engineering and Technology
- Teofilo Kisanji University
- Teofilo Kisanji University Tabora Centre
- Tumaini University, Mbeya Centre
- Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMCo)
2.0 Aidha, kutokana na mapungufu katika vyuo mbalimbali imeamriwa kwamba jumla ya programu 75 kutoka vyuo 22 nchini zimesitishwa kudahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18. Kuona Programu ambazo zimesitishwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/18 tafadhali bonyeza hapa.
3.0 Aidha Tume inapenda kusisitiza kwamba, uamuzi huu hautawahusu wanafunzi wanaondelea na masomo katika programu na vyuo husika.
Imetolewa na:
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
24 Julai 2017
3.0 Aidha Tume inapenda kusisitiza kwamba, uamuzi huu hautawahusu wanafunzi wanaondelea na masomo katika programu na vyuo husika.
Imetolewa na:
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
24 Julai 2017
No comments:
Post a Comment