Arsenal imepata ushindi wa mechi 3 mfululizo kwa mara ya kwanza - www.gbgraphixpro.com

Random Posts

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Arsenal imepata ushindi wa mechi 3 mfululizo kwa mara ya kwanza

Share This

Baada ya headlines za muda mrefu kuhusu mwenendo na kiwango kibovu cha Arsenalkatika mashindano mbalimbali wakiwa chini ya kocha wao mfaransa Arsene Wenger, mchezo wa nusu fainali ya FA Cup dhidi ya Man City waliyopata ushindi wa magoli 2-1 umeonekana kuleta morali katika kikosi cha timu hiyo.
Arsenal usiku wa April 26 walikuwa wenyeji wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu EnglandLeicester City katika uwanja wao wa Emirates kucheza mchezo wao wa 32 wa Ligi KuuEngland msimu huu, Arsenal wao wanahangaika kumaliza katika TOP 4 ili wapate nafasi ya kucheza Champions League wakati Leicester wanajaribu kujinusuru na wimbi la kushuka daraja.
Katika game hiyo ambayo Arsenal alikuwa nyumbani wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 baada ya Robert Huth wa Leicester kujifunga dakika ya 87 ya mchezo kutokana na kugongwa na shuti lililopigwa na Ignacio Monreal, hii inakuwa ni mara ya kwanza kwaArsenal kupata ushindi katika mechi tatu mfululizo za mashindano tofauti toka January 2017.
Kama utakuwa unakumbuka Arsenal alipata ushindi wa 2-1 wa FA dhidi ya Man CityApril 23, mchezo dhidi ya Middlesbrough wa 2-1 April 17 na leo amefanikiwa kupata ushindi wa 3 dhidi ya LeicesterArsenal  sasa itarudi uwanjani Jumapili ya April 30 wakiwa ugenini kucheza dhidi ya Tottenham wakati Leicester City watakuwa ugenini April 29 kucheza dhidi ya West Bromwich Albion.

No comments:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages